Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 8

Al-Hujuraat 49:8

الحجرات

فَضْلًا مِّنَ ٱللَّهِ وَنِعْمَةً ۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. [8]

[8] Na hiyo ni fadhila tukufu na neema kubwa ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kwa ujuzi wake, ni Mwenye hikima ya kupita mpaka katika kuendesha kila jambo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kheri hii walioipata ni fadhila kutoka kwa Allah Mtukufu juu yao na ni neema. Na Allah Mtukufu Anamjua vizuri anayezishukuru neema Zake, ni Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo ya viumbe Vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net