Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 7

Al-Hujuraat 49:7

الحجرات

وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ فِيكُمْ رَسُولَ ٱللَّهِ ۚ لَوْ يُطِيعُكُمْ فِى كَثِيرٍ مِّنَ ٱلْأَمْرِ لَعَنِتُّمْ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ ٱلْإِيمَـٰنَ وَزَيَّنَهُۥ فِى قُلُوبِكُمْ وَكَرَّهَ إِلَيْكُمُ ٱلْكُفْرَ وَٱلْفُسُوقَ وَٱلْعِصْيَانَ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلرَّٰشِدُونَ

Maana

Na jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeliwatii katika mambo mengi, bila ya shaka mngelitaabika. Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezea Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amewafanya muuchukie ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walioongoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeli kut'iini katika mambo mengi, bila ya shaka mngeli taabika. Lakini Mwenyezi Mungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amekufanyeni muuchukie ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walio ongoka! [7]

[7] Na jueni, enyi Waumini, kwamba Mtume yuko nanyi. Basi mkadirieni kama anavyo stahiki kadiri yake, na msadikini. Lau yeye angeli wafuata walio wachache wa Imani kati yenu katika mambo mengi, basi hapana shaka mngeli ingia katika mashaka na hilaki. Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezesha Imani wale walio kamilika katika nyinyi, na akaipamba katika nyoyo zenu. Basi jilindeni na kujipamba na yasiyo takikana. Na amekufanyeni mchukie kukufuru neema za Mwenyezi Mungu, na kutokana na sharia zake, na kwenda kinyume na amri zake. Hao tu, peke yao, ndio wanao ijua njia ya uwongofu na wameishikilia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mjue kuwa baina yenu yupo Mtume wa Allah Mtukufu, kuweni na adabu naye, kwani yeye anayajua zaidi mambo yanayowafaa kuliko nyinyi, anawatakia kheri, na nyinyi huenda mkajitakia shari na madhara ambayo Mtume hawakubalii, na lau yeye angewafuata nyinyi katika mengi mnayoyachagua, hilo lingepelekea muingie kwenye usumbufu. Lakini Allah Mtukufu Amewafanya muipende Imani na Akaifanya ipambike ndani ya nyoyo zenu ndipo mkaamini, na Amewafanya mchukie kumkanusha Allah Mtukufu, na kutoka nje ya twaa Yake na kumuasi. Hao waliosifika kwa sifa hizi ndio waongofu wenye kufuata njia ya haki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net