Al-Hujuraat 49:10
الحجراتإِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا۟ بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe. [10]
[10] Hakika wote wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni ndugu, Imani imezifanya nyoyo zao pamoja. Basi patanisheni baina ya ndugu zenu kwa kufuata udugu wa Imani. Na jiwekeeni nafsi zenu kinga cha kukinga adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kufuata amri yake, na kuepuka anayo yakataza, na huku mkitaraji Mwenyezi Mungu akurehemuni kwa uchamngu wenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Waumini ni ndugu katika Dini, basi fanyeni upatanishi baina ya ndugu zenu wawili wakipigana. Na mwogopeni Allah Mtukufu katika mambo yenu yote, kwa kutarajia mrehemewe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net