Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 4

Al-Hujuraat 49:4

الحجرات

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَآءِ ٱلْحُجُرَٰتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ

Maana

Hakika hao wanaokuita nawe uko nyuma ya vyumba, wengi wao hawatumii akili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika hao wanao kuita nawe uko nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili. [4]

[4] Hakika hao wanao kuita kwa makelele nawe uko vyumbani mwako wengi wao hawafahamu yanayo takikakana kukuhishimu na kukutukuza kwa makamo yako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale wanaokuita, (ewe Nabii), nyuma ya vyumba vyako kwa sauti ya juu, wengi wao hawana akili ya kuwapelekea kuwa na adabu nzuri pamoja na Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na kumheshimu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net