Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 5

Al-Hujuraat 49:5

الحجرات

وَلَوْ أَنَّهُمْ صَبَرُوا۟ حَتَّىٰ تَخْرُجَ إِلَيْهِمْ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na lau wao wangelingojea mpaka uwatokee, ingelikuwa heri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwingi wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau wao wangeli ngojea mpaka uwatokee ingeli kuwa kheri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu. [5]

[5] Na lau kuwa hao wangeli ngojea, kwa kukufanyia adabu, mpaka ukatoka, bila ya shaka ingeli kuwa ni bora zaidi katika Dini yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kusamehe, Mwenye rehema kunjufu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau wangesubiri mpaka ukawatokea ingekua bora zaidi kwao mbele ya Allah Mtukufu, kwa kuwa Allah Mtukufu Amewaamrisha kukuheshimu. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa yale yaliyotokea kwao ya madhambi na utovu wa adabu kwa kutojua kwao, ni Mwingi wa rehema kwao kwa kutowaharakishia mateso.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net