Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 48 · Aya ya 28

Al-Fath 48:28

الفتح

هُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلْهُدَىٰ وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا

Maana

Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aipe ushindi juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yeye Ndiye Aliyemtuma Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa ubainufu ulio wazi na Dini ya Uislamu, ili aifanye kuwa juu ya mila zote. Na Allah Mtukufu anatosha kuwa ni shahidi kwamba Yeye ni Mwenye kukupa ushindi na kuidhihirisha Dini yako juu ya kila dini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Fath

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net