Al-Fath 48:27
الفتحلَّقَدْ صَدَقَ ٱللَّهُ رَسُولَهُ ٱلرُّءْيَا بِٱلْحَقِّ ۖ لَتَدْخُلُنَّ ٱلْمَسْجِدَ ٱلْحَرَامَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَ ۖ فَعَلِمَ مَا لَمْ تَعْلَمُوا۟ فَجَعَلَ مِن دُونِ ذَٰلِكَ فَتْحًا قَرِيبًا
Hakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah (Mwenyezi Mungu akipenda), kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele. Hamtakuwa na hofu. Yeye anajua msiyoyajua. Basi atawapea kabla ya haya Ushindi karibuni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah, kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele. Hamtakuwa na khofu. Yeye anajua msiyo yajua. Basi atakupeni kabla ya haya Ushindi karibuni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika Allah Mtukufu Alimsadikishia Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ndoto yake aliyomuotesha kwa haki kwamba utaingia, wewe na Maswahaba wako, Nyumba takatifu ya Allah Mtukufu hali ya kuwa mko katika amani, hamuwaogopi watu wa ushirikina, hali ya kuwa mnanyoa vichwa vyenu na mnapunguza. Allah Mtukufu Alijua kheri na maslahi ya kuwaepusha nyinyi na Makkah mwaka wenu huo na kuingia baadae, msiyoyajua, na Akajaalia, kabla ya kuingia kwenu (Makkah) mliyoahidiwa, ya ushindi wa karibu, (nao ni mapatano ya amani ya Ḥudaybiyah na ushindi wa ufunguzi wa Khaybar).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net