Al-Fath 48:26
الفتحإِذْ جَعَلَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى قُلُوبِهِمُ ٱلْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ ٱلْجَـٰهِلِيَّةِ فَأَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ وَأَلْزَمَهُمْ كَلِمَةَ ٱلتَّقْوَىٰ وَكَانُوٓا۟ أَحَقَّ بِهَا وَأَهْلَهَا ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمًا
Pale wale waliokufuru walipotia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga, Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini, na akawalazimisha neno la kumcha Mungu. Na wao walikuwa ndio wenye haki nalo na wenye kustahili. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua mno kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Pale walio kufuru walipo tia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga, Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini, na akawalazimisha neno la kuchamngu. Na wao walikuwa ndio wenye haki nalo na wenye kustahili. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wangeadhibiwa hao waliokufuru pindi walipoingiza ndani ya nyoyo zao wivu wa watu wa zama za ujinga, ili wasikubali utume wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na miongoni mwa hayo ni kule kukataa kwao kuandika «Bi ism Allāh al-Raḥmān al-Raḥīm» katika mapatano ya Ḥudaybiyah, na wakakataa kuandika, «Haya ndiyo yale aliyoyapitisha Muhammad, Mtume wa Allah Mtukufu.» Na Allah Mtukufu Akamteremshia utulivu Mtume Wake na Waumini aliokua nao, Akawathibitishia neno «Lā ilāha illā Allāh» ambalo ndilo kichwa cha kila uchamungu. Na Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na Waumini ndio wanaostahiki zaidi neno la uchamungu kuliko washirikina. Na hivyo ndivyo walivyokuwa, walistahiki neno hili na sio washirikina. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa ujuzi wa kila kitu, hakuna kitu chochote kinachofichika Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net