Al-Fath 48:25
الفتحهُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوكُمْ عَنِ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ وَٱلْهَدْىَ مَعْكُوفًا أَن يَبْلُغَ مَحِلَّهُۥ ۚ وَلَوْلَا رِجَالٌ مُّؤْمِنُونَ وَنِسَآءٌ مُّؤْمِنَـٰتٌ لَّمْ تَعْلَمُوهُمْ أَن تَطَـُٔوهُمْ فَتُصِيبَكُم مِّنْهُم مَّعَرَّةٌۢ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ لِّيُدْخِلَ ٱللَّهُ فِى رَحْمَتِهِۦ مَن يَشَآءُ ۚ لَوْ تَزَيَّلُوا۟ لَعَذَّبْنَا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا
Hao ndio waliokufuru na wakawazuia msiingie Msikiti Mtakatifu, na wakawazuilia dhabihu kufika mahala pao. Na lau si wanaume Waumini na wanawake Waumini msiowajua mkawasaga na mkaingia makosani kutokana nao bila ya kujua... Mwenyezi Mungu (amefanya haya) ili amuingize amtakaye katika rehema yake. Lau wangelitengana, bila ya shaka tungeliwaadhibu wale waliokufuru kwa adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio walio kufuru na wakakuzuieni msiingie Msikiti Mtakatifu, na wakawazuilia dhabihu kufika mahala pao. Na lau si wanaume Waumini na wanawake Waumini msio wajua mkawasaga na mkaingia makosani kutokana nao bila ya kujua Mwenyezi Mungu (amefanya haya) ili amuingize amtakaye katika rehema yake. Lau wangeli tengana bila ya shaka tungeli waadhibu walio kufuru kwa adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Makafiri wa Kikureshi ndio waliokataa kumpwekesha Allah Mtukufu, wakawazuia nyinyi, (Siku ya Ḥudaybiyah), kuingia Msikiti wa (al-Ḥarām), wakakataza wanyama na wakawafunga wasifike mahali pa wao kuchinjwa, (napo ni Ḥaram). Na lau si wanaume Waumini walio wanyonge na wanawake Waumini msiowajua, walio kati ya hawa makafiri wa (Makkah), wanaoificha Imani yao kwa kuzichelea nafsi zao, msije mkawakanyaga kwa jeshi lenu mkawaua, mkapata dhambi, aibu na gharama kwa mauaji hayo bila kujua, tungewapa nyinyi uwezo juu yao, ili Allah Mtukufu Apate kumtia kwenye rehema Zake Anayemtaka, kwa kumpa neema ya kuamini badala ya kukanusha. Lau hawa Waumini wa kiume na Waumini wa kike wangejitenga na washirikina wa Makkah na wakajitoa kati yao, tungewaadhibu wale waliokufuru na kukanusha miongoni mwao adhabu yenye uchungu na kuumiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net