Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 48 · Aya ya 24

Al-Fath 48:24

الفتح

وَهُوَ ٱلَّذِى كَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ عَنْهُم بِبَطْنِ مَكَّةَ مِنۢ بَعْدِ أَنْ أَظْفَرَكُمْ عَلَيْهِمْ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا

Maana

Na Yeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu, na mikono yenu kwao, katika bonde la Makka baada ya kuwapeni Ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno myatendayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Yeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu, na mikono yenu kwao, katika bonde la Makka baada ya kukupeni Ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona myatendayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Yeye Ndiye Aliyeizuia mikono ya washirikina isiwafikie nyinyi, na mikono yenu isiwafikie wao katika bonde la Makkah baada ya nyinyi kuwakamata wao wakawa chini ya mamlaka yenu. (washirikina hawa ndio wale walioenda kuishambulia kambi ya askari wa Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), hapo (Ḥudaybiyah), Waislamu wakawakamata kisha wakawaachia, na walikuwa ni kiasi cha wanaume themanini.) Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyaona matendo yenu, hakuna chochote kinachofichika Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Fath

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net