Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 48 · Aya ya 11

Al-Fath 48:11

الفتح

سَيَقُولُ لَكَ ٱلْمُخَلَّفُونَ مِنَ ٱلْأَعْرَابِ شَغَلَتْنَآ أَمْوَٰلُنَا وَأَهْلُونَا فَٱسْتَغْفِرْ لَنَا ۚ يَقُولُونَ بِأَلْسِنَتِهِم مَّا لَيْسَ فِى قُلُوبِهِمْ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ لَكُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا إِنْ أَرَادَ بِكُمْ ضَرًّا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ نَفْعًۢا ۚ بَلْ كَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًۢا

Maana

Watakuambia mabedui waliobaki nyuma: 'Zimetushughulisha mali zetu na ahali zetu, basi tuombee msamaha.' Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwamo katika nyoyo zao. Sema: 'Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kuwadhuru au akitaka kuwanufaisha? Bali Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watakuambia mabedui walio baki nyuma: Yametushughulisha mali yetu na ahali zetu, basi tuombee msamaha. Wanasema kwa ndimi zao yasiyo kuwamo katika nyoyo zao. Sema: Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kukudhuruni au akitaka kukunufaisheni? Bali Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watakwambia, ewe Nabii, wale mabedui waliojikalisha nyuma wasitoke na wewe kwenda Makkah utakapowalaumu, «Tulishughulishwa na mali zetu na watu wa nyumbani kwetu, basi tuombee Mola Wako Atusamehe kosa letu la kujikalisha nyuma.» Wanasema hayo kwa ndimi zoa na hayana ukweli wowote maneno yao ndani ya nyoyo zao. Waambie, «Ni nani atakayemiliki na kuwafanyia chochote zaidi ya Allah Mtukufu iwapo Allah Mtukufu atawatakia nyinyi kheri au shari?» mambo sivyo kama vile hawa wanafiki wanavyodhania kuwa Allah Mtukufu hayajui yale ya unafiki yaliyomo ndani yao. Bali kwa hakika, Yeye Allah Mtukufu ni Mtambuzi wa mnayoyafanya, hakuna chochote kinachofichika Kwake katika matendo ya viumbe Vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Fath

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net