Al-Fath 48:10
الفتحإِنَّ ٱلَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ ٱللَّهَ يَدُ ٱللَّهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَـٰهَدَ عَلَيْهُ ٱللَّهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا
Bila ya shaka wale wanaokupa kiapo cha utii, kwa hakika wanampa Mwenyezi Mungu kiapo cha utii. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Kwa hivyo, avunjaye ahadi hizi, basi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake. Na anayetekeleza aliyomuahadi Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Basi avunjaye ahadi hizi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake; na anaye tekeleza aliyo muahadi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika hao wanaokupa mkono, ewe Mtume, wa ahadi ya kupigana hapo (Ḥudaybiyah), wao kwa kweli wanampa mkono wa ahadi Allah Mtukufu na wanafanya mapatano na Yeye kwa kutaka Pepo Yake na radhi Zake. Mkono wa Allah Mtukufu uko juu ya mikono yao. Hivyo basi Yupo na wao anayasikia maneno yao, Anawaona mahali walipo na Anayajua mambo yao ya ndani na ya nje. Basi mwenye kuivunja ahadi yake aliyoitolea mkono, maangamivu ya jambo hilo yatamrudia mwenyewe; na atakayetekeleza ahadi aliyomuahidi Allah Mtukufu ya kuvumilia wakati wa mapambano na adui katika njia ya Allah Mtukufu na kumnusuru Nabii wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), Allah Mtukufu Atampa malipo mema mengi, nayo ni Pepo. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya mkono kwa Allah Mtukufu kwa namna inayonasibiana naye Aliyetakasika, bila kufananisha wala kueleza ulivyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net