Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 48 · Aya ya 12

Al-Fath 48:12

الفتح

بَلْ ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَنقَلِبَ ٱلرَّسُولُ وَٱلْمُؤْمِنُونَ إِلَىٰٓ أَهْلِيهِمْ أَبَدًا وَزُيِّنَ ذَٰلِكَ فِى قُلُوبِكُمْ وَظَنَنتُمْ ظَنَّ ٱلسَّوْءِ وَكُنتُمْ قَوْمًۢا بُورًا

Maana

Lakini mlidhani kwamba Mtume na Waumini hawatarudi kabisa kwa ahali zao, na mkapambiwa hayo katika nyoyo zenu, na mkadhania dhana mbaya, na mkawa watu wanaoangamia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini mlidhani kwamba Mtume na Waumini hawatarudi kabisa kwa ahali zao, na mkapambiwa hayo katika nyoyo zenu, na mkadhania dhana mbaya, na mkawa watu wanao angamia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Pia mambo sivyo kama mlivyodai kuwa mlishughulishwa na mali na watu wa nyumbani, bali kwa kweli nyinyi mlidhani kuwa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na wale Maswahaba waliokuwa naye wataangamia na hawatarudi kwenu kabisa, na Shetani aliwapambia hilo ndani ya nyoyo zenu. Na pia mlidhani dhana mbaya kuwa Allah Mtukufu Hatampa ushindi Nabii Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na Maswahaba wake juu ya maadui wao, na mmekua ni watu wenye kuangamia msiokuwa na kheri yoyote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Fath

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net