Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 38

Muhammad 47:38

محمد

هَـٰٓأَنتُمْ هَـٰٓؤُلَآءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَمِنكُم مَّن يَبْخَلُ ۖ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِۦ ۚ وَٱللَّهُ ٱلْغَنِىُّ وَأَنتُمُ ٱلْفُقَرَآءُ ۚ وَإِن تَتَوَلَّوْا۟ يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوٓا۟ أَمْثَـٰلَكُم

Maana

Angalieni! Nyinyi hawa mnaitwa mtumie mali katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanaofanya ubahili. Na anayefanya ubahili, basi anajifanyia ubahili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka, atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi. [38]

[38] Hivi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu aliyo iamrisha. Kati yenu wapo wanao fanya ubakhili kutoa. Na mwenye kufanya ubakhili hamdhuru mtu ila nafsi yake. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye tajiri, hana haja ya mtu, na nyinyi ndio mafakiri wenye kumhitajia Yeye. Na mkiacha kumt'ii Mwenyezi Mungu basi atakubadilisheni pahala penu awalete watu wengine, tena hao hawatakuwa mfano wenu wa kuacha kumt'ii.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haya nyinyi, enyi Waumini, mnaitwa kutoa kwenye kupigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu na kuinusuru Dini Yake. Basi miongoni mwenu kuna anayefanya uchoyo kutoa katika njia ya Allah Mtukufu. Na mwenye kufanya uchoyo huwa anajifanyia uchoyo nafsi yake. Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Mkwasi wa kutowahitajia nyinyi, na nyinyi ndio mnaomhitajia Yeye. Na mkiipa mgongo haki, mkaacha kumuamini Allah Mtukufu na kufuata amri Zake, Atawaangamiza na Atawaleta watu wengine, na kisha wasiwe ni kama nyinyi katika kuzipa mgongo amri za Allah Mtukufu, bali wao watamtii Yeye na kumtii Mtume Wake, na watapigana jihadi katika njia Yake kwa mali yao na nafsi zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net