Al-Fath 48:1
الفتحإِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا
Hakika sisi tumekufungulia Ushindi wa dhahiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika tumekufungulia Ushindi wa dhaahiri .
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tumekufungulia wewe (tumekupa ushindi), ewe Mtume, ushindi ulio wa dhahiri, ambao ndani yake Allah Mtukufu Ataipa nguvu Dini yake na Atakupa ushindi juu ya maadui wako, na ushindi huo ni mapatano ya (Ḥudaybiyah), ambayo kwayo watu waliingia katika amani, na zikapanuka juhudi za ulinganizi wa Dini ya Allah Mtukufu, na watu wakaingia kwenye Dini ya Allah Mtukufu makundi kwa makundi. Kwa sababu hiyo, Allah Mtukufu Aliyaita mapatano hayo “ushindi ulio wa wazi” yaani uliokuwa wazi wenye kujitokeza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net