Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 37

Muhammad 47:37

محمد

إِن يَسْـَٔلْكُمُوهَا فَيُحْفِكُمْ تَبْخَلُوا۟ وَيُخْرِجْ أَضْغَـٰنَكُمْ

Maana

Na akikutakeni hizo na kukushikilieni, mtafanya ubahili, na atatoa undani wa chuki zenu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na akikutakeni hayo na kukushikilieni mtafanya ubakhili, na atatoa undani wa chuki zenu. [37]

[37] Akikutakeni na akakushikilieni basi nyinyi mtafanya uchoyo, na chuki zenu zitaonekana kwa mnavyo yapenda mali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Anapowataka mtoe mali zenu na kuwahimiza kwenye hilo mnafanya ubahili na mnakataa kutoa. Na anapowataka mtoe mali mnayochukia kuitoa mnadhihirisha chuki na uhasidi wa nyoyo zenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net