Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 35

Muhammad 47:35

محمد

فَلَا تَهِنُوا۟ وَتَدْعُوٓا۟ إِلَى ٱلسَّلْمِ وَأَنتُمُ ٱلْأَعْلَوْنَ وَٱللَّهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَـٰلَكُمْ

Maana

Basi msilegee na mkataka suluhu, maana nyinyi ndio mtakaoshinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatawanyima malipo ya vitendo vyenu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu. [35]

[35] Basi msijifanye wanyonge mbele ya maadui zenu mnapo kutana nao. Wala msiwatake suluhu kwa kuwaogopa, na hali nyinyi ndio mko juu, na ni wenye kushinda kwa nguvu za Imani. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi kwa nusra yake; na wala hatakupunguzieni malipo ya vitendo vyenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi msiwe wanyonge, enyi wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, wa kujiepusha na kupambana na washirikina, mkaogopa kupigana nao, na mkawaita kwenye suluhu na masikilizano na hali ya kuwa nyinyi ndio wenye ushindi na nguvu juu yao, na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Yuko pamoja na nyinyi kwa kuwanusuru na kuwapa nguvu. Hapa kuna bishara kubwa ya kupatiwa ushindi na kusaidiwa juu ya maadui. Na Allah Mtukufu Hatawapunguzia malipo mema ya matendo yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net