Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 34

Muhammad 47:34

محمد

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ مَاتُوا۟ وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يَغْفِرَ ٱللَّهُ لَهُمْ

Maana

Hakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao. [34]

[34] Hakika walio kufuru na wakazuia watu wasiingie katika Uislamu, kisha wakafa nao ni makafiri, basi Mwenyezi Mungu hatawasamehe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale waliokataa kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, na wakawazuia watu na Dini Yake, kisha wakafa wakiwa katika hali hiyo, Allah Mtukufu Hatawasamehe, na Atawapa adhabu ikiwa ndio mateso yao kwa ukanushaji wao, na Atawafedhehesha mbele ya halaiki ya watu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net