Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 3

Muhammad 47:3

محمد

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱتَّبَعُوا۟ ٱلْبَـٰطِلَ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّبَعُوا۟ ٱلْحَقَّ مِن رَّبِّهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ أَمْثَـٰلَهُمْ

Maana

Hayo ni kwa sababu wale waliokufuru wamefuata upotovu, na wale walioamini wamefuata Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata upotovu, na walio amini wamefuata Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo wapigia watu mifano yao. [3]

[3] Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata njia ya upotovu, na kwamba walio amini wamefuata njia ya Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Kwa mfano kama huu wa kubainisha kwa uwazi ndio Mwenyezi Mungu anawaeleza watu hali zao ili wapate kuzingatia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kupoteza huko na kuongoza, sababu yake ni kwamba wale waliokufuru wamemfuata Shetani wakamtii, na kwamba wale walioamini walimfuata Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na yale aliyokuja nayo ya mwangaza na uongofu. Kama Alivyobainisha Allah Mtukufu vile Anavyoyafanya mapote mawili ya watu wa ukafiri na watu wa Imani kwa wanavyostahili, vilevile Allah Mtukufu, Aliyetakasika, Anawapigia watu mifano yao, ili kila watu wanaofanana (wa aina moja) wakutane na wale wanaonasibiana nao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net