Muhammad 47:2
محمدوَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَءَامَنُوا۟ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۙ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّـَٔاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ
Na wale walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini yale aliyoteremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio amini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyo teremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao. [2]
[2] Na walio amini, na wakatenda mema, na wakasadiki yaliyo teremshwa kwa Muhammad, nayo ni Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, atawafutia makosa yao, na atawatengenezea hali yao ya Dini na dunia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale waliomuamini Allah Mtukufu na wakafuata Sheria Zake na wakaamini Kitabu Alichomteremshia Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), nacho ndicho ukweli usiokuwa na shaka kutoka kwa Mola wao, Allah Mtukufu Atawasamehe maovu waliyoyafanya na hatawatesa kwa maovu hayo, na atawatengenezea mambo yao duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net