Muhammad 47:25
محمدإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱرْتَدُّوا۟ عَلَىٰٓ أَدْبَـٰرِهِم مِّنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلْهُدَى ۙ ٱلشَّيْطَـٰنُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَىٰ لَهُمْ
Kwa hakika wale wanaorudi nyuma baada ya uongofu kwisha wabainikia, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika wanao rudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri. [25]
[25] Hakika wale walio ritadi, wakarejea nyuma kwenye ukafiri na upotofu walio kuwa nao baada ya kuwadhihirikia njia ya uwongofu, Shetani ndiye aliye wapambia, na akawakunjulia matamanio ya uwongo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliyorudi nyuma wakaacha uongofu na Imani na wakageuka kwa visigino vyao wakimkanusha Allah Mtukufu baada ya haki kuwadhihirikia, hao Shetani amewapambia makosa yao na akawanyoshea matumaini ya kuishi duniani muda mrefu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net