Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 26

Muhammad 47:26

محمد

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا۟ لِلَّذِينَ كَرِهُوا۟ مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ سَنُطِيعُكُمْ فِى بَعْضِ ٱلْأَمْرِ ۖ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ

Maana

Hayo ni kwa sababu waliwaambia wale waliochukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu: 'Tutakutiini katika baadhi ya mambo.' Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu waliwaambia walio chukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu: Tutakut'iini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao. [26]

[26] Kurejea huko ukafirini ni kwa kuwa waliwaambia wenye kuchukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu: Tutakut'iini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anazijua siri za hawa wanaafiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kule kuwapa muda wao hadi wakakomaa kwenye ukafiri, ni kwa kuwa walisema kuwaambia Mayahudi waliokanusha Aliyoyateremsha Allah Mtukufu, «Tutawatii katika baadhi ya mambo ambayo yako kinyume na amri ya Allah Mtukufu na amri ya Mtume Wake.» Na Allah Mtukufu Aliyetukuka Anayajua wanayoyaficha na wanayoydhihirisha. Basi Muislamu ajihadhari na kumtii asiyekuwa Allah Mtukufu katika mambo yaliyo kinyume na amri ya Allah Mtukufu, Aliyetakasika, na amri ya Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net