Muhammad 47:24
محمدأَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ ٱلْقُرْءَانَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَآ
Je, hawaizingatii hii Qur-ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli zake?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli? [24]
[24] Wameingia upofu hata hawaufahamu uwongofu wa Qur'ani? Bali kwenye nyoyo zao zipo kufuli zinawazuia wasiizingatie.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, si wayazingatie mawaidha ya Qur’ani wanafiki hawa na wazifikirie hoja zake? Lakini nyoyo hizi zimefungwa, hakuna chochote katika maana za hii Qur’ani kinacho ingia kwenye nyoyo zao, hivyo basi haziyatii akilini mawaidha ya Allah Mtukufu na mazingatio yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net