Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 23

Muhammad 47:23

محمد

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰٓ أَبْصَـٰرَهُمْ

Maana

Hao ndio aliowalaani Mwenyezi Mungu, na akawatia uziwi, na akawapofua macho yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao. [23]

[23] Hao ndio alio watenga mbali kabisa Mwenyezi Mungu na rehema yake, na akawatia uziwi wasiisikie Haki, na akawatia upofu wa macho wasiione Njia ya Uwongofu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio ambao Allah Mtukufu Amewaepusha na rehema zake, Akawafanya wasiyasikie yanayowanufaisha na wasiyaone, na pia zisiwadhihirikie hoja za Allah Mtukufu pamoja na kuwa ni nyingi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net