Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 9

Al-Ahqaf 46:9

الأحقاف

قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ ٱلرُّسُلِ وَمَآ أَدْرِى مَا يُفْعَلُ بِى وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ وَمَآ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ

Maana

Sema: 'Mimi si kitu kigeni miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyofanywa mimi wala nyinyi. Mimi nafuata niliyofunuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji wa wazi wazi.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi. [9]

[9] Waambie: Mimi sikuwa Mtume wa mwanzo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hata ndio muukatae ujumbe wangu. Wala mimi sijui Mwenyezi Mungu atanifanya nini na atakufanyeni nini nyinyi. Mimi sifuati ninayo sema au kutenda ila anayo nifunulia Mwenyezi Mungu. Wala mimi si chochote ila ni mwonyaji miongoni mwa waonyaji.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, uwaambie washirikina wa watu wako, “Sikuwa wa mwanzo wa wajumbe wa Allah Mtukufu kwa viumbe Wake. Na sijui Atakalofanya Mwenyezi Mngu kwangu wala kwenu hapa duniani. Sifuati katika yale ninayowaamrisha nyinyi na katika yale ninayoyafanya isipokuwa wahyi wa Allah Mtukufu Anaoniletea. Na sikuwa isipokuwa ni mwenye kuonya ambaye uonyaji wake uko wazi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net