Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 10

Al-Ahqaf 46:10

الأحقاف

قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ وَكَفَرْتُم بِهِۦ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّنۢ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ عَلَىٰ مِثْلِهِۦ فَـَٔامَنَ وَٱسْتَكْبَرْتُمْ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Sema: 'Mnaonaje yakiwa haya ni kweli yametoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi mmeyakufuru, na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini, na nyinyi mnafanya kiburi? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mwaonaje yakiwa haya ni kweli yametoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi mmeyakataa, na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini, na nyinyi mnafanya kiburi? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. [10]

[10] Sema: Hebu nambieni, ikiwa hii Qur'ani inatoka kwa Mwenyezi Mungu na nyinyi mkaikataa, na hali ameshuhudia shahidi katika Wana wa Israili kuwa imeshuka mfano wa hii kutoka kwa Mwenyezi Mungu, akawa yeye kaamini na nyinyi mkatakabari, basi hapo nyinyi si mtakuwa ni wenye kupotea na wenye kujidhulumu wenyewe kuliko watu wote? Hakika Mwenyezi Mungu hamsaidii kuongoka mwenye kujidhulumu mwenyewe na akapanda kiburi kuikataa Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, uwaambie washirikina wa watu wako, “Nipasheni habari: ikiwa hii Qur’ani inatoka kwa Allah Mtukufu na mkaikanusha, na hali ameshuhudia shahidi kati ya Wana wa Isrãîl, kama ‘Abdullāh bin Salām, kwa mfano wa hii Qur’ani, nayo ni yaliyomo ndani ya Taurati ya kusadikisha unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), akaiamini na akayafuata kivitendo yaliyokuja ndani ya Qur’ani, na nyinyi mkakanusha hilo kwa njia ya kiburi, Basi hamuoni kuwa hiki mnachokifanya si chochote isipokuwa ni udhalimu mkubwa na ukafiri mwingi?” Hakika Allah Mtukufu Hawaongozi kwenye Uislamu na kuifikia haki wale watu waliojidhulumu kwa kumkanusha Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net