Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 11

Al-Ahqaf 46:11

الأحقاف

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَوْ كَانَ خَيْرًا مَّا سَبَقُونَآ إِلَيْهِ ۚ وَإِذْ لَمْ يَهْتَدُوا۟ بِهِۦ فَسَيَقُولُونَ هَـٰذَآ إِفْكٌ قَدِيمٌ

Maana

Na wale waliokufuru waliwaambia wale walioamini: 'Lau kuwa hii ni heri, wasingelitutangulia kuifikia.' Na walipokosa kuongoka, wakasema: 'Huu ni uzushi mkubwa wa zamani.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walio kufuru waliwaambia walio amini: Lau kuwa hii ni kheri, wasingeli tutangulia. Na walipo kosa kuongoka wakasema: Huu ni uzushi wa zamani. [11]

[11] Na walio kufuru walisema kuwakhusu walio amini, kwa kejeli na majivuno juu yao: Ingeli kuwa aliyo kuja nayo Muhammad ni ya kheri, basi wasingeli tutangulia hawa katika kuyaamini. Kwani sisi ndio twenye ubwana, na akili bora! Na ilivyo kuwa hawakuyafuata basi wakaangukia kuyatoa kombo, wakisema: Huu ni uwongo wa zamani unatokana na hadithi za watu wa kale!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale walioukanusha unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), walisema wakiwaambia wale waliomuamini, “Lau huko kumuamini Muhammad kwa aliyokuja nayo ni kheri msingetutangulia kuamini.” Na kwa kuwa hawakujiongoza na hii Qur’ani wala hawakunufaika na ukweli uliomo ndani yake, watasema, Huu ni urongo uliopokewa kwa watu wa kale.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net