Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 12

Al-Ahqaf 46:12

الأحقاف

وَمِن قَبْلِهِۦ كِتَـٰبُ مُوسَىٰٓ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ وَهَـٰذَا كِتَـٰبٌ مُّصَدِّقٌ لِّسَانًا عَرَبِيًّا لِّيُنذِرَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ وَبُشْرَىٰ لِلْمُحْسِنِينَ

Maana

Na kabla yake kilikuwapo Kitabu cha Musa, chenye uongozi na rehema. Na hiki ni Kitabu cha kusadikisha na kilichokuja kwa lugha ya Kiarabu, ili kiwaonye wale waliodhulumu, na kiwe ni bishara njema kwa watendao mema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kabla yake kilikuwapo Kitabu cha Musa, kuwa chenye uwongozi na rehema. Na hichi ni Kitabu cha kusadikisha na kilicho kuja kwa lugha ya Ki./Arabu, ili kiwaonye walio dhulumu, na kiwe ni bishara kwa watendao mema. [12]

[12] Na kabla ya Qur'ani Mwenyezi Mungu aliteremsha Taurati kuwa ni uwongozi na rehema kwa wenye kuitenda. Na hii Qur'ani wanayo ikadhibisha inasadikisha Vitabu vilivyo kwisha tangulia. Mwenyezi Mungu ameiteremsha kwa lugha ya Kiarabu iwe ni onyo jipya kwa wenye kudhulumu, na bishara kwa wenye kusimama sawa juu ya Njia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kabla ya hii Qur’ani, tuliiteremsha Taurati ikiwa ni muongozo kwa Wana wa Isrãîl waifuate na ni rehema kwa wenye kuiamini na kuifuata kivitendo. Na hii Qur’ani inasadikisha Vitabu vilivyokuwa kabla yake. Tumeiteremsha kwa lugha ya Kiarabu ili iwaonye wale waliozidhulumu nafsi zao kwa kukanusha na kuasi. Na bishara njema ni ya wale waliomtii Allah Mtukufu na wakafanya wema katika Imani yao na utiifu wao duniani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net