Al-Ahqaf 46:13
الأحقافإِنَّ ٱلَّذِينَ قَالُوا۟ رَبُّنَا ٱللَّهُ ثُمَّ ٱسْتَقَـٰمُوا۟ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Hakika wale waliosema: 'Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu' kisha wakanyooka sawasawa, hawatakuwa na hofu, wala hawatahuzunika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu; kisha wakatengenea, hawatakuwa na khofu, wala hawatahuzunika. [13]
[13] Hakika wanao sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu peke yake, kisha wakatengenea kwa kufanya vitendo vizuri, watu hao hawana khofu ya kushukiwa la karaha, na wala hawatahuzunika kwa kuyakosa wayatakayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliosema, “Mola wetu ni Allah Mtukufu” kisha wakathibiti katika kumuamini, basi hao hawatakuwa na khofu ya kubabaika Siku ya Kiyama na ya vitisho vyake, wala hawatasikitika juu ya hadhi za duniani walizoziacha nyuma yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net