Al-Ahqaf 46:14
الأحقافأُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ خَـٰلِدِينَ فِيهَا جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Hao ndio watu wa Bustani za mbinguni, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio watu wa Peponi, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. [14]
[14] Hao wanao sifika kwa kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja, na kusimama sawa, ndio walio khusika kuingia Peponi wakikaa humo milele. Mwenyezi Mungu amewapa hayo kuwa ni jaza yao kwa mema waliyo kuwa wakiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao ni wa watu wa Peponi, watakaa humo milele kwa rehema za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, juu yao, na kwa yale waliyoyatanguliza ya matendo mema katika dunia yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net