Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 8

Al-Ahqaf 46:8

الأحقاف

أَمْ يَقُولُونَ ٱفْتَرَىٰهُ ۖ قُلْ إِنِ ٱفْتَرَيْتُهُۥ فَلَا تَمْلِكُونَ لِى مِنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَا تُفِيضُونَ فِيهِ ۖ كَفَىٰ بِهِۦ شَهِيدًۢا بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ ۖ وَهُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Maana

Au wanasema: 'Ameizua mwenyewe!' Sema: 'Ikiwa nimeizua mimi, basi nyinyi hamwezi kunifaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Yeye anajua zaidi hayo mnayoropokwa; anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Na Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au wanasema: Ameizua mwenyewe! Sema: Ikiwa nimeizua mimi, basi nyinyi hamwezi kunifaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Yeye anajua zaidi hayo mnayo ropokwa; anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Na Yeye ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [8]

[8] Bali wanasema hawa makafiri: Muhammad ameizua hii na akamsingizia Mwenyezi Mungu! Sema kuwajibu: Ikiwa mimi nimeizua hii Mwenyezi Mungu atanipatiliza upesi upesi, wala nyinyi hamwezi kunilinda hata kwa chembe ya adhabu. Yeye peke yake ndiye Mwenye kujua kabisa hayo mnayo ropokwa katika kuzitia kombo Aya zake. Na Yeye anatosha kunishuhudia ukweli wangu, na kukushuhudilieni nyinyi kuwa mnanikadhibisha. Na Yeye pekee, ndiye Mkunjufu wa msamaha kwa mwenye kutubu, Mkubwa wa rehema, kwa kuwapa muhula wenye kuasi ili wadiriki kurejea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au je wanasema hawa washirikina kwamba Muhammad ameizua Qur’ani? Waambie, ewe mtume, “Iwapo mimi nimemzulia Allah Mtukufu hii Qur’ani, basi nyinyi hamuwezi kunikinga mimi na adhabu ya Allah Mtukufu kitu chochote Akiwa atanitesa kwa hilo. Yeye, kutakasika ni Kwake, ni Mjuzi zaidi wa kile mnachokisema juu ya hii Qur’ani kuliko kitu chochote kingine. Inatosha kuwa Allah Mtukufu ni Shahidi juu yangu mimi na nyinyi, na Yeye Ndiye Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwingi wa rehema kwa waja Wake Waumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net