Al-Ahqaf 46:5
الأحقافوَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُۥٓ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ وَهُمْ عَن دُعَآئِهِمْ غَـٰفِلُونَ
Na ni nani mpotovu mkubwa kuliko hao wanaoomba badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama, na wala hata hawatambui maombi yao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanao waomba, badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama, na wala hawatambui maombi yao. [5]
[5] Na nani aliye zidi kupotea kuliko anaye muacha Mwenyezi Mungu akaiomba miungu mingine ambayo haitamjibu kitu mpaka mwisho wa dunia, na ambao hao hata hawana khabari ya maombi yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna aliyepotea zaidi wala aliye mjinga zaidi kuliko yule anayewaomba waungu wengine badala ya Allah Mtukufu, waungu wasioitikia maombi yake kabisa mpaka Siku ya Kiyama, kwa kuwa waungu hao ni wafu au mawe au miti na mfano wa hivyo, na hali hivyo havina habari ya maombi ya huyo mwenye kuviabudu, havina uwezo wa kumnufaisha au kumdhuru.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net