Al-Ahqaf 46:6
الأحقافوَإِذَا حُشِرَ ٱلنَّاسُ كَانُوا۟ لَهُمْ أَعْدَآءً وَكَانُوا۟ بِعِبَادَتِهِمْ كَـٰفِرِينَ
Na ambao watu watakapokusanywa watakuwa maadui zao, na wataikataa ibada yao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ambao watu watakapo kusanywa watakuwa maadui zao, na wataikataa ibada yao. [6]
[6] Na watu wakikusanywa kwa ajili ya hisabu Siku ya Kiyama hawa wanao abudiwa kwa upotovu watakuwa ndio maadui wa walio kuwa wakiabudu, na watajitenga nao, na kuwakadhibisha kwa madai yao kwamba wao wanastahiki kuabudiwa. (Katika Injili ya Mathayo inasimuliwa wazi vipi Nabii Isa a.s. atavyo wakataa Wakristo wanao muabudu yeye. Tazama Mathayo 7.22-23. Yesu anasema: "Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.")
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pindi watu watakapokusanywa Siku ya Kiyama ili wahesabiwe na walipwe, wale waungu waliokuwa wakiwaomba duniani watakuwa ni maadui zao, wakiwalaani na kujiepusha nao na kukanusha kuwa wao walikuwa wanajua kuwa wale wanawaabudu wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net