Al-Ahqaf 46:4
الأحقافقُلْ أَرَءَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَرُونِى مَاذَا خَلَقُوا۟ مِنَ ٱلْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ ۖ ٱئْتُونِى بِكِتَـٰبٍ مِّن قَبْلِ هَـٰذَآ أَوْ أَثَـٰرَةٍ مِّنْ عِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Sema: Je, mwawaona wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Nionyesheni wameumba nini katika ardhi; au hao wanalo fungu katika mbingu zote? Nileteeni Kitabu kilichokuwa kabla ya hiki, au alama yoyote ya elimu, ikiwa mnasema kweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Mwawaona wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu? Nionyesheni wameumba nini katika ardhi; au hao wanayo shirika katika mbingu? Nileteeni Kitabu kilicho kuwa kabla ya hiki, au alama yoyote ya ilimu, ikiwa mnasema kweli. [4]
[4] Waambie hao wanao muomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu: Hebu nambieni hali ya hao mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu. Nijuvyeni wameumba nini katika ardhi, au wana ushirika wowote katika mbingu? Nileteeni Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu, au mabaki yoyote kutokana na ilimu za watu wa zamani ambayo mnayategemea kwa madai yenu, ikiwa mnasema kweli.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa makafiri, “Hivi mnawaona waungu na masanamu mnaowaabudu badala ya Allah Mtukufu? Hebu nionesheni, ni sehemu gani waliyoiumba katika ardhi? Au kwani wao wana fungu katika uumbaji mbingu? Nileteeni kitabu kinachotoka kwa Allah Mtukufu kabla ya hii Qur’ani au mabaki yaliyosalia ya elimu, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net