Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 3

Al-Ahqaf 46:3

الأحقاف

مَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ عَمَّآ أُنذِرُوا۟ مُعْرِضُونَ

Maana

Hatukuziumba mbingu na ardhi wala yaliyo baina yake ila kwa haki na kwa muda maalumu. Na wale waliokufuru wanayapuuza yale wanayoonywa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hatukuziumba mbingu na ardhi wala yaliyomo baina yake ila kwa haki na kwa muda maalumu. Na walio kufuru wanayapuuza yale wanayo onywa. [3]

[3] Hatukuziumba mbingu na ardhi na vyote vilio baina yake ila kufuatana na sharia zilizo thibiti, kwa makusudio yanayo ambatana na hikima, na kwa muda maalumu ambao baada yake utakwisha. Na wale wanao ukataa ukweli huu wanapuuza yale waliyo onywa kwayo, ya kuumbwa kupya siku watakapo fufuliwa watu kwa ajili ya malipo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina ya viwili hivyo isipokuwa kwa haki, si kwa mchezo na upuuzi, bali tumeziumba ili waja wapate kujua ukubwa wa Muumba wa hizo na wamuabudu Peke Yake na wajue kuwa Yeye ni Muweza wa kuwarudishia waja uhai baada ya kufa kwao, na ili wasimamishe haki na uadilifu baina yao, mpaka ufike wakati huo unaojulikana Kwake. Na wale waliokanusha kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mungu wa Kweli, wanayapa mgongo yale ambayo Qur’ani inawaonya kwayo; wao hawawaidhiki wala hawafikirii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net