Al-Ahqaf 46:35
الأحقاففَٱصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُو۟لُوا۟ ٱلْعَزْمِ مِنَ ٱلرُّسُلِ وَلَا تَسْتَعْجِل لَّهُمْ ۚ كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَ مَا يُوعَدُونَ لَمْ يَلْبَثُوٓا۟ إِلَّا سَاعَةً مِّن نَّهَارٍۭ ۚ بَلَـٰغٌ ۚ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلَّا ٱلْقَوْمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ
Basi subiri, kama walivyosubiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayoyaona hayo waliyoahidiwa, itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipokuwa watu wavukao mipaka tu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayo yaona waliyo ahidiwa itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipo kuwa walio waovu tu? [35]
[35] Ewe Muhammad! Wastahamilie makafiri kama walivyo stahamili Mitume wengine wenye nguvu na imara wakati wa shida. Wala usiwahimizie adhabu. Kwani hiyo itawafika tu, hapana hivi wala hivi, hata ikichukua muda mrefu. Siku watapo kiona kitisho chake watadhani kuwa hawakukaa kabla yake ila saa moja tu ya mchana. Haya uliyo watolea waadhi yatosha. Hawataangamizwa kwa adhabu isipo kuwa walio toka kwenye ut'iifu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi vumilia, ewe Mtume, kwa yanayokupata ya maudhi ya watu wako wenye kukukanusha kama vile walivyovumilia Mitume wenye nia thabiti kabla yako wewe, nao, kwa kauli mashuhuri, ni Nūḥ, Ibrãhîm, Mûsã na Ῐsā, na wewe ni miongoni mwao, wala usiwafanyie haraka watu wako ya kuadhibiwa. Kwani itakapotokea na wakaiona, watajihisi kana kwamba hawakukaa duniani isipokuwa muda mchache wa mchana. Huu ni ujumbe kwao na kwa wasiokuwa wao. Na hawaangamizwi kwa adhabu ya Allah Mtukufu isipokuwa watu waliotoka nje ya amri Yake na twaa Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net