Al-Ahqaf 46:34
الأحقافوَيَوْمَ يُعْرَضُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ عَلَى ٱلنَّارِ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِٱلْحَقِّ ۖ قَالُوا۟ بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا۟ ٱلْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ
Na siku watakapoletwa makafiri Motoni, wakaambiwa: 'Je, haya si kweli?' Watasema: 'Ndivyo? Tunaapa kwa Mola wetu Mlezi, ni kweli!' Atasema: 'Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyokuwa mkikufuru.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na siku watakapo letwa makafiri Motoni wakaambiwa: Je! Haya si kweli? Watasema: Kwani? Tunaapa kwa Mola wetu Mlezi, ni kweli! Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya kule kukataa kwenu. [34]
[34] Na siku watakapo simamishwa walio kufuru Motoni wataambiwa kwa kukemewa: Adhabu hii si jambo la kweli linakubaliana na tuliyo kuonyeni nayo duniani? Na wao watasema: Kwani? Tunaapa kwa Mola wetu Mlezi, haya ni haki kweli. Atasema: Onjeni kila namna ya adhabu kali kwa kushikilia kwenu ukafiri na ukanushi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Siku ya Kiyama, wataorodheshwa waliokufuru juu ya Moto wa Jahanamu ili waadhibiwe na waambiwe, «Hivi hii adhabu si kweli?». watajibu kwa kusema, «Ndio. Tunaapa kwa Mola wetu kuwa hii ndiyo kweli.» Hapo waambiwe, «Basi onjeni adhabu kwa kuwa mlikuwa mkiikataa adhabu ya Moto na kuikanusha duniani».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net