Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 33

Al-Ahqaf 46:33

الأحقاف

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَلَمْ يَعْىَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَـٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحْـِۧىَ ٱلْمَوْتَىٰ ۚ بَلَىٰٓ إِنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Je, hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliyeziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu? Kwani? Hakika Yeye ni Muweza mno wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliye ziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu? Kwani? Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu. [33]

[33] Wameghafilika wala hawajui kwamba Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi, na wala hakushindwa kuziumba, ni Muweza wa kuwafufua maiti? Bali Yeye ni Muweza wa hayo, kwani Yeye Mtukufu ana uweza kaamili juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, wameghafilika na wasijue kwamba Allah Mtukufu, Aliyeumba mbingu na ardhi pasi na mfano uliotangulia na bila kuelemewa na kuziumba, ni Muweza wa kuhuisha wafu ambao Aliwaumba hapo mwanzo? Ndio, hilo ni jambo jepesi kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka, Ambaye hakuna chochote kinachomshinda. Hakika Yeye kwa kila jambo ni Muweza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net