Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 32

Al-Ahqaf 46:32

الأحقاف

وَمَن لَّا يُجِبْ دَاعِىَ ٱللَّهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَيْسَ لَهُۥ مِن دُونِهِۦٓ أَوْلِيَآءُ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

Maana

Na wasiomwitikia Mwitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wasio mwitikia Mwitaji wa Mwenyezi Mungu basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhaahiri. [32]

[32] Na asiye muitikia Mwenyezi Mungu basi hawezi kumshinda Mwenyezi Mungu asimtie mkononi hata akikimbia vipi katika ardhi. Na wala hana isipo kuwa Mwenyezi Mungu wa kumnusuru na kumkinga na adhabu yake. Hao wanao puuza wasimwitikie mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu wamo katika ubabaishi na dhaahiri wako mbali na Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na asiyemuitikia Mtume wa Allah Mtukufu katika yale aliyoyalingania, basi yeye hatamshinda Allah Mtukufu katika ardhi Akitaka kumuadhibu, wala hatakuwa na wasaidizi badala ya Allah Mtukufu, wenye kumkinga na adhabu Yake. Hao watakuwa wametoka nje ya haki waziwazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net