Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 31

Al-Ahqaf 46:31

الأحقاف

يَـٰقَوْمَنَآ أَجِيبُوا۟ دَاعِىَ ٱللَّهِ وَءَامِنُوا۟ بِهِۦ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

Maana

Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu, na muaminini, Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawakinga kutokana na adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu, na muaminini, Mwenyezi Mungu atakusameheni, na atakukingeni na adhabu chungu. [31]

[31] Enyi watu wetu! Muitikieni mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu anaye ongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka. Na msadikini Mwenyezi Mungu akusameheni madhambi yenu yaliyo tangulia, na akulindeni na adhabu kali iliyo chungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi jamaa zetu! Muitikieni Mtume wa Allah Mtukufu Muhammad kwa kile anachowaitia, na muaminini yeye na myafuate kivitendo yale aliyoyaleta, Allah Mtukufu Atawasamehe dhambi zenu na Atawaokoa na adhabu yenye uchungu inayoumiza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net