Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 30

Al-Ahqaf 46:30

الأحقاف

قَالُوا۟ يَـٰقَوْمَنَآ إِنَّا سَمِعْنَا كِتَـٰبًا أُنزِلَ مِنۢ بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِىٓ إِلَى ٱلْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ

Maana

Wakasema: 'Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa, kinachosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake, na kinachoongoza kwenye Haki na kwenye njia iliyonyooka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka. [30]

[30] Walisema: Enyi watu wetu! Hakika sisi tumekisikia Kitabu chenye shani kubwa. Kimeteremshwa baada ya Musa, na kinasadikisha Vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyo tangulia, kinaongoza kwenye itikadi ya haki, na sharia ya vitendo iliyo simama sawa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walisema, «Enyi jamaa zetu! Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Mûsã, chenye kusadikisha Vitabu vya Allah Mtukufu vilivyokuwa kabla yake, ambavyo Allah Mtukufu Ameviteremsha kwa Mitume Wake, Kitabu ambacho kinaongoza kwenye haki na usawa na kwenye njia sahihi iliyonyooka».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net