Al-Ahqaf 46:29
الأحقافوَإِذْ صَرَفْنَآ إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ ٱلْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ ٱلْقُرْءَانَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوٓا۟ أَنصِتُوا۟ ۖ فَلَمَّا قُضِىَ وَلَّوْا۟ إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ
Na wakati tulipowaleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur-ani. Basi walipoihudhuria, walisema: 'Sikilizeni!' Na ilipokwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakati tulipo waleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur'ani. Basi walipo ihudhuria walisema: Sikilizeni! Na ilipo kwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya. [29]
[29] Ewe Muhammad! Taja tulipo kuletea kikundi cha majini waje sikiliza Qur'ani. Walipo hudhiria ilipo kuwa ikisomwa, baadhi yao wakawaambia wenzao: Sikilizeni! Ilipo kwisha timia kusomwa wakarudi kwa haraka kwa wenzao, kuwahadharisha na ukafiri, wakiwataka waamini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipokutumia kundi la majini kusikiliza Qur’ani kutoka kwako. Walipohudhuria, na Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), yuwasoma, waliambiana wao kwa wao, Nyamazeni tusikilize Qur’ani! Na Mtume Alipomaliza kusoma Qur’ani, na wao wakawa wameielewa na ikawa imewaathiri, walirudi kwa majini wenzao wakawaonya na kuwatahadharisha na adhabu ya Allah Mtukufu wasipoamini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net