Al-Ahqaf 46:28
الأحقاففَلَوْلَا نَصَرَهُمُ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ قُرْبَانًا ءَالِهَةًۢ ۖ بَلْ ضَلُّوا۟ عَنْهُمْ ۚ وَذَٰلِكَ إِفْكُهُمْ وَمَا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ
Basi mbona wale waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu, kuwa ati hao ndio wawakurubishe, hawakuwanusuru? Bali waliwapotea! Na huo ndio uongo mkubwa waliokuwa wakiuzua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi mbona wale walio washika badala ya Mwenyezi Mungu, kuwa ati hao ndio wawakurubishe, hawakuwanusuru? Bali waliwapotea! Na huo ndio uwongo walio kuwa wakiuzua. [28]
[28] Basi kwani hao walio wafanya miungu badala ya Mwenyezi Mungu ili iwakaribishe kwa Mwenyezi Mtukufu imeweza kuwakinga na maangamizo? Hasha! Bali miungu hiyo iliwakimbia, na hali wao ndio wana haja nayo mno iwanusuru. Na hayo yaliyo wafika, ya kutupwa na miungu yao, na kuwapotea ndio matokeo ya uwongo wao na uzushi wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi si wangewasaidia, hao tuliowaangamiza miongoni mwa ummah waliopita, waungu wao ambao walifanya kule kuwaabudu kwao ni ibada ya wao kujikurubisha kwa Mola wao, ili wawaombee mbele Yake. Lakini waungu wao waliwapotea, hawakuwaitikia wala hawakuwatetea. Huo ni urongo wao tu na uzushi walioupanga wa kuwafanya wao ni waungu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net