Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 27

Al-Ahqaf 46:27

الأحقاف

وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا مَا حَوْلَكُم مِّنَ ٱلْقُرَىٰ وَصَرَّفْنَا ٱلْـَٔايَـٰتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

Maana

Na hakika tuliiangamiza miji iliyo jirani zenu, na tulizitumia Ishara mbalimbali ili wapate kurejea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tuliiangamiza miji ilio jirani zenu, na tulizitumia Ishara ili wapate kurejea. [27]

[27] Enyi watu wa Makka! Tumeiangamiza miji iliyo jirani zenu. Na Sisi tuliwawekea wazi dalili namna mbali mbali, ili wapate kurejea waache ukafiri. Hawakurejea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tuliiangamiza miji iliyokuwa pembezoni mwenu, enyi watu wa Makkah, kama ile ya kina ‛Ᾱd na Thamūd, tukazifanya kuta za nyumba za miji hiyo zimeanguka na kulalia sakafu zake zilizovunjika, na tuliwabainishia watu wa miji hiyo aina za hoja na dalili, wapate kurudi nyuma na kuyaacha yale waliokuwa nayo ya ukanushaji Allah Mtukufu na aya Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net