Al-Ahqaf 46:26
الأحقافوَلَقَدْ مَكَّنَّـٰهُمْ فِيمَآ إِن مَّكَّنَّـٰكُمْ فِيهِ وَجَعَلْنَا لَهُمْ سَمْعًا وَأَبْصَـٰرًا وَأَفْـِٔدَةً فَمَآ أَغْنَىٰ عَنْهُمْ سَمْعُهُمْ وَلَآ أَبْصَـٰرُهُمْ وَلَآ أَفْـِٔدَتُهُم مِّن شَىْءٍ إِذْ كَانُوا۟ يَجْحَدُونَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
Na bila ya shaka tuliwaweka vizuri siyo kama tulivyokuwekeni nyinyi, na tuliwapa uwezo wa kusikia, na kuona na ufahamu wa nyoyo. Na hayakuwafaa uwezo wao wa kusikia, na kuona na ufahamu wa nyoyo kwa lolote. Kwani hao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara ndiyo yakawafika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na bila ya shaka tuliwaweka vizuri sio kama tulivyo kuwekeni nyinyi; na tuliwapa masikio, na macho, na nyoyo. Na hayakuwafaa kitu masikio yao, wala macho yao, wala nyoyo zao kwa lolote. Kwani hao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na yale waliyo kuwa wakiyafanyia maskhara ndiyo yakawazunguka. [26]
[26] Na tuliwaweka kabila la A'di kwa nafasi na nguvu sio kama tulivyo kuwekeni nyinyi watu wa Makka. Na tuliwajaalia masikio, na macho, na nyoyo, lau wangeli taka kunafiika kwayo. Lakini hayakuwafaa hata kitu kidogo masikio yao, wala macho yao, wala nyoyo zao, kwa sababu walikuwa wakizikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu. Basi hayo yakapinga baina yao na kunafiika kwa waliyo letewa. Na ile ile adhabu waliyo kuwa wakiifanyia maskhara ikawazunguka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwarahisishia hao ‛Ᾱd sababu za kumakinika duniani kwa namna ambayo hatukuwamakinisha nyinyi, enyi makureishi, na tuliwafanya wawe na masikio ya kusikia na macho ya kuonea na nyoyo za kufahamia, wakavitumia katika mambo yanayomfanya Allah Mtukufu Awe na hasira nao. Na hilo halikuwafaa kitu chochote kwa kuwa walikuwa wakikanusha hoja za Allah Mtukufu, na adhabu ambayo walikuwa wakiifanyia shere na kuiharakisha. Hili ni onyo kutoka kwa Allah Mtukufu, imetukuka shani Yake, na ni tahadharisho kwa wenye kukufuru.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net