Al-Ahqaf 46:25
الأحقافتُدَمِّرُ كُلَّ شَىْءٍۭ بِأَمْرِ رَبِّهَا فَأَصْبَحُوا۟ لَا يُرَىٰٓ إِلَّا مَسَـٰكِنُهُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْقَوْمَ ٱلْمُجْرِمِينَ
Unaharibu kila kitu kwa amri ya Mola wake Mlezi. Wakawa hawaonekani ila nyumba zao tu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo watu wahalifu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Unaangamiza kila kitu kwa amri ya Mola wake Mlezi. Wakawa hawaonekani ila nyumba zao tu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wakosefu! [25]
[25] Itakayo teketeza kila kitu kwa amri ya Muumbaji wake. Nao ukawaangamiza, yasionekane mabaki yao isipo kuwa nyumba zao. Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kutenda kama makosa yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Unaangamiza kila kitu unachokipitia katika vitu ambavyo ulitumwa uviangamize kwa amri ya Mola wake na matakwa Yake. Wakawa hakuna kinachoonekana chochote katika miji yao isipokuwa nyumba zao walizokuwa wakizikaa. Mfano wa malipo haya ndiyo tunayowalipa makafiri kwa sababu ya uhalifu wao na kupita kiasi kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net