Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 24

Al-Ahqaf 46:24

الأحقاف

فَلَمَّا رَأَوْهُ عَارِضًا مُّسْتَقْبِلَ أَوْدِيَتِهِمْ قَالُوا۟ هَـٰذَا عَارِضٌ مُّمْطِرُنَا ۚ بَلْ هُوَ مَا ٱسْتَعْجَلْتُم بِهِۦ ۖ رِيحٌ فِيهَا عَذَابٌ أَلِيمٌ

Maana

Basi walipoliona wingu likielekea kwenye mabonde yao, walisema: 'Hili ni wingu la kutunyeshea mvua!' Kumbe sivyo, haya ni hayo mliyotaka yawajie haraka: upepo ambao ndani yake imo adhabu chungu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi walipo liona wingu likielekea kwenye mabonde yao, walisema: Wingu hili la kutunyeshea mvua! Kumbe sivyo, haya ni hayo mliyo yahimiza, upepo ambao ndani yake imo adhabu chungu! [24]

[24] Ikawajia adhabu kwa sura ya wingu. Walipo liona limetanda kote juu linaelekea mabondeni kwao, walisema kwa furaha: Wingu hili linatuletea mvua na kheri. Wakaambiwa: Bali hilo ni hayo mliyo yahimiza, nayo ni upepo wenye adhabu kali na chungu, itakayo teketeza kila kitu kwa amri ya Muumbaji wake. Nao ukawaangamiza, yasionekane mabaki yao isipo kuwa nyumba zao. Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kutenda kama makosa yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walipoiona adhabu walioifanyia haraka imejitokeza juu ikielekea kwenye mabonde yao, walisema, “Hiki ni kiwingu chenye kutunyesheza mvua.” Hûd, amani imshukie, aliwaambia, «Hiki si kiwingu cha mvua na rehema kama mlivyodhania, bali hiki ni kiwingu cha adhabu mliyoitaka kwa haraka, huo ni upepo ambao ndani yake muna adhabu yenye uchungu na yenye kuumiza».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net