Al-Ahqaf 46:23
الأحقافقَالَ إِنَّمَا ٱلْعِلْمُ عِندَ ٱللَّهِ وَأُبَلِّغُكُم مَّآ أُرْسِلْتُ بِهِۦ وَلَـٰكِنِّىٓ أَرَىٰكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ
Akasema: 'Hakika ujua wa hayo uko kwa Mwenyezi Mungu. Mimi nawafikishieni yale niliyotumwa nayo. Lakini nawaona kuwa nyinyi mnafanya ujinga tu.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Hakika ujuzi uko kwa Mwenyezi Mungu. Mimi nakufikishieni niliyo tumwa. Lakini nakuoneni kuwa nyinyi mnafanya ujinga. [23]
[23] Hud akasema: Ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kujua wakati wa kuileta adhabu yenu. Mimi nafikisha ujumbe tu nilio tumwa. Lakini naona kuwa nyinyi hamjui chochote katika mambo wanayo tumwa Mitume.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hûd, amani imshukie, akasema, Hakika ujuzi wa adhabu mliyoahidiwa uko kwa Allah Mtukufu, na kwa kweli mimi ni Mtume wa Allah Mtukufu kwenu, ninawafikishia ujumbe Alionituma nao, ila mimi ninawaona kuwa ni watu mlio wajinga kwa kuifanyia haraka adhabu na kuwa na ujasiri juu ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net