Al-Ahqaf 46:18
الأحقافأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ ٱلْقَوْلُ فِىٓ أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ خَـٰسِرِينَ
Hao ndio ambao imehakikishwa hukumu juu yao kama mataifa yaliyokwisha pita kabla yao miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa wenye kuhasiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio ambao imehakikikishwa hukumu juu yao kama mataifa yaliyo kwisha pita kabla yao miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa wenye kukhasiri. [18]
[18] Hao wasemao hayo ndio iliyo wathibitikia kuwashukia adhabu sawa sawa na mataifa yaliyo kuwa kabla yao miongoni mwa majini na watu, kwa sababu hakika hao walikuwa ni wenye kukhasiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao ambao sifa zao ni hizi imepasa juu yao adhabu ya Allah Mtukufu, na yamewashukia mateso Yake na hasira Zake, wakiwa ni katika jumla ya ummah waliopita kabla yao, miongoni mwa majini na binadamu, waliokuwa kwenye ukafiri na ukanushaji. Kwa kweli wao ni wenye hasara kwa kuchagua upotevu na kuacha uongofu, na kuchagua adhabu na kuacha starehe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net