Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 19

Al-Ahqaf 46:19

الأحقاف

وَلِكُلٍّ دَرَجَـٰتٌ مِّمَّا عَمِلُوا۟ ۖ وَلِيُوَفِّيَهُمْ أَعْمَـٰلَهُمْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

Maana

Na wote watakuwa na daraja zao mbalimbali kwa waliyoyatenda, na ili awalipe kwa ukamilifu kwa vitendo vyao, na wala hawatadhulumiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wote watakuwa na daraja zao mbali mbali kwa waliyo yatenda, na ili awalipe kwa vitendo vyao, na wala hawatadhulumiwa. [19]

[19] Na wote, Waislamu na makafiri, wana vyeo vyao vinavyo lingana na vitendo vyao walivyo vitenda, ili uadilifu wa Mwenyezi Mungu upate kuonekana kati yao, na ili awalipe jaza ya 'amali zao, nao hawatadhulumiwa, kwa sababu wanastahiki hayo wanayo lipwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kila kundi la watu wema na watu waovu watakuwa madaraja mbalimbali mbele ya Allah Mtukufu Siku ya Kiyama, kwa matendo yao waliyoyatenda duniani, kila mmoja kulingana na daraja yake, ili Allah Mtukufu Awatekelezee malipo ya matendo yao. Na wao hawatadhulumiwa kwa kuongezewa maovu yao wala kupunguziwa mema yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net